Activity Report

Muziki Unaongea 🎶
Muziki Unaongea 🎶
@efmtanzania
Followers: 4,908,879Posts: 85,680Following: 3
📻 93.7 Dsm | 93.9 Moshi | 103.7 Arusha | 94.1 Iringa | 91.3 Mwanza | 88.9 Tanga | 92.5 Dodoma | 95.5 Moro | 102.9 Kigoma | 103.3 Mbeya | 93.7 ZNZ 📻
View all posts from @efmtanzania
Maisha ni mabadiliko ya kila siku... CLUB SILVER PIPE (Nyuma ya 777 bar, njia ya Kwenda Lugalo Golf Course) inazinduliwa upyaaaa kabisaaaa.

Ni Jumamosi ya tarehe 2 mwezi wa Nane 2025 saa kumi na mbili asubuhi, Tutaanza na Fun Run ya kilomita 5 na Kilomita 10 tukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe @smtambule 

#EDigitalUpdates
1 72
Karibu Katika #JotoLaAsubuhiEFM

Tufuatilie live kwenye Youtube channel yetu EFM TANZANIA weka maoni yako yatasomwa hewani.

Cc  @irenekillenga @kipandee_ @fatmalikwata @rdj_mafuta @zuberi_mkalaboko @ibrahim_ambokilee 

💻 @eddomobby 
✍️ @bigthemadness 

#JotoLaAsubuhiEFM
1 29
Usajili wa Yanga ni usajili wa mapungufu - Mkalaboko

Cc: @ibrahim_ambokilee @zuberi_mkalaboko 

#ESports
49 4152 61021
Nilianza kuuza Pochi pasipo na mtaji wa Biashara - 🗣@bitemapochi

Cc: #MiriamMlaponi #NancyIbrahim #Salma

#LadiesLoungeEFM
4 203 10764
Biriani bila Vitunguu Bado halijakamilika - @mpishii_ Bwana Emmanuel Victor anasema ni kweli Biriani bila Vitunguu litakuwa bado halijakamilika.

Cc: #MiriamMlaponi #NancyIbrahim #Salma

#LadiesLoungeEFM
4 253 12028
Jinsi ya kupika Birian tamu lenye ladha, Huyu hapa  @mpishii_ Bwana Emmanuel Victor anafafanua kiundani kuhusu upishi wa Biriani tamu.

Cc: #MiriamMlaponi #NancyIbrahim #Salma

#LadiesLoungeEFM
7 266 11858
Utamaduni wa Hiphop hubeba upendo,amani na Heshima, @afandesele1976 amepokea heshima za @therealfidq  huku nae akimzungumza namna ambavyo aliheshimu uwepo wake tangu siku ya kwanza.

Tazama mahojiano haya kwa kugusa link kwenye bio hapo juu 

Nb : usikose tukio la heshima kwa Afande Sele la @bongoflavahonors siku ya tarehe 1 Aug 2025 pale The Cask 

#Theclassicefmnaafandesele #Theclassicefm #everythingclassic
46 1886 32177
Mahusiano mazuri ya kidiplomasia na ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Canada umeendelea kuipaisha sekta ya Afya nchini hivyo kuboresha zaidi ubora wa huduma za afya ngazi ya msingi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Julai 20, 2025 mara baada ya kumpokea Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai pamoja na ujumbe aliyoambatana nao kutoka nchini Canada waliowasili kwa lengo la kufanya ziara ya siku tano nchini.

“Tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Canada kwa kuendelea kuwa mshirika wa maendeleo ya sekta ya Afya nchini Tanzania, kwa mchango wanaoutoa kwenye mfuko wa pamoja wa afya (Health Basket Fund) ambao unasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya ngazi ya msingi kupitia mfumo wa ufadhili wa moja kwa moja katika vituo vya Afya awamu ya kwanza (2022–2027)” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amebainisha kuwa Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Canada katika kuboresha huduma za afya ya uzazi, haki za vijana balehe pamoja na kuimarisha huduma za uuguzi wakati wa kujifungua ambazo zinalenga kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwa kuongeza upatikanaji wa wakunga wenye ujuzi. 

“Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Canada katika sekta ya afya umeleta mafanikio mengi ikiwemo kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 67 mwaka 2015 hadi asilimia 43 mwaka 2022 kwa kila vizazi hai 1,000, kupungua kwa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kutoka 556 hadi 104 kwa kila vizazi hai laki 100,000” amefafanua Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama hakusita kuelezea changamoto ya kasi ndogo ya kupungua kwa vifo vya watoto wachanga, kutoka vifo 25 kwa kila vizazi hai elfu 1,000 mwaka 2015 hadi vifo 24 kwa kila vizazi hai elfu 1,000 mwaka 2022 na kutumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya Canada kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza afua za afya zinazolenga kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai ameshukuru kwa mapokezi mazuri nchini Tanzania na ameahidi nchi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika Sekta ya Afya. 

#EDigitalUpdates
4 293
Mashindano ya CECAFA Ratiba kusogezwa Mbele.
-
Mwenyekiti chama cha soka mkoa wa Arusha ndugu Zakayo Mjema analithibitisha hili kwenye mazungumzo na Game Plan sababu ikiwa ni timu ya Senegal kuchelewa kuwasili.
-
Mashindano haya yaliyotarajiwa kuanza kesho yatahusisha mataifa manne ya ukanda wa CECAFA na Senegal ikiwemo, tayari mpaka sasa  Tanzania, Kenya zimeshawasili.

Cc @majid83tz 

💻 @iammaroon14
2 1053 42002
Kuhusu mchezaji nyota Elie Mpanzu Meneja Mawasiliano Simba @ahmedally_ anasema haya.

"Mcheziji tukimuacha sisi ndio anaweza kwenda kwenye hiyo timu nyingine, hapa Tanzania hakuna timu inayoweza kununua mkataba wa Mpanzu"
-
Uchambuzi kwa urefu upo kwenye youtube yetu EFM TANZANIA kupitia Game Plan

Cc @majid83tz @tiganatz @salumumnolela 

💻 @iammaroon14
77 10260 168666
Benki ya CRDB imetangazwa kuwa Benki Bora Tanzania, Benki Bora kwa Masuala ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG), na Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati (SME) na jarida la kifedha la kimataifa la Euromoney, wakati wa hafla ya kutuza washindi wa Tuzo za Ubora za Euromoney iliyofanyika jijini London Julai 17 2025. 

Tuzo hizo zilipokelewa kwa niaba ya Benki na Bi. Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, katika hafla iliyohudhuriwa na zaidi ya wabobezi 500 wa sekta ya benki na fedha kutoka kote duniani. Bi. Mwambapa aliambatana na maafisa waandamizi wa Benki ya CRDB pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Bi. Mwambapa alisema, "Heshima hii ya tuzo nne kutoka Euromoney inadhihirisha dhamira ya msingi ya Benki yetu ya kuwa mshirika wa kweli wa maendeleo kwa watu binafsi, wafanyabiashara, na jamii kwa ujumla.

"Tunapoendelea na kuadhimisha miaka 30 ya Benki ya CRDB, tuzo hizi zinatupa chachu ya kuendelea kusimamia kusudi letu la kuboresha maisha na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu katika uendeshaji wetu."

Tuzo hizi tatu zimekuja miezi miwili tu baada ya Benki ya CRDB kutambuliwa na Euromoney kama Benki Bora kwa huduma za benki zinazofata misingi ya Kiislamu nchini Tanzania kupitia huduma zake za CRDB Al Barakah Banking wakati wa tuzo za Euromoney Islamic Finance zilizofanyika Dubai mnamo tarehe 20 Mei 2025 na kufanya Benki ya CRDB kubeba jumla ya tuzo nne kutoka Euromoney tuzo zenye heshima kubwa zaidi katika sekta ya fedha ulimwenguni.

#EDigitalUpdates
4 288
Mchambuzi wa masuala ya Siasa na Mwanazuoni Dkt. Dennis Muchunguzi anasema utaratibu uliotumika kumteua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea Urais kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulikuwa halali na hakuna taratibu iliyovunjwa;

Kwani baada ya jina lake kupendekezwa na wajumbe wa mkutano mkuu, vikao vyote vya kamati kuu na Halmashauri kuu vilikaa ili kuleta majina ya wagombea.

Dkt. Muchunguzi anayasema hayo kwenye Podcast ya Kikao cha Dharura akiwa na @speshokabwanga

#EDigitalUpdates
122 468 33846