Activity Report

Jambo Online Tv
Jambo Online Tv
@jambo_online_tv
Followers: 1,105,708Posts: 22,396Following: 0
News&Media website
View all posts from @jambo_online_tv
VIDEO:

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amewasili viunga vya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwenye Kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali za Chama hicho.

Leo Julai 28, 2025, Jaji Hamidu Mwanga anatarajiwa kutoa uamuzi utakaotoa hatima yake kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo ya madai ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohammed, Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Zanzibar na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.

Walalamikiwa kwenye kesi hiyo ni Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho.
1 52 635
VIDEO:

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amewasili katika viunga vya Mahakama Kuu – Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kwenye kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali za chama hicho.

Leo, Julai 28, 2025, Jaji Hamidu Mwanga anatarajiwa kutoa uamuzi muhimu kuhusu iwapo ataendelea kusikiliza kesi hiyo ama la.

Kesi hiyo ya madai ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohammed (Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Zanzibar) pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho upande wa Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa na Katibu Mkuu wa Chadema.
15 395 4826
VIDEO:

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza, ametumia jukwaa la mkutano wa ndani wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) katika Kata ya Kisukuru, Jimbo la Segerea, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam kutoa hoja nzito za kuwataka wananchi kuwapa nafasi ya miaka mitano ili kuthibitisha uwezo wa chama hicho katika kuleta mabadiliko ya kweli nchini.

Akizungumza siku ya Jumapili, Kaiza, ambaye sasa ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa na ujasiri wa kujaribu kitu kipya badala ya kung’ang’ania kile ambacho kimeshindwa kwa miaka mingi.

Akifananisha hali hiyo na mpangaji anayeamua kuhama nyumba chakavu na kujaribu nyumba nyingine mpya, Kaiza alisema kuwa hata kama nyumba mpya haitaridhisha, bado mpangaji ana uhuru wa kurudi nyumba ya zamani. Kwa mantiki hiyo, aliwataka wananchi kuwakopesha CHAUMMA imani ya miaka mitano tu.

Kaiza pia aliwakumbusha wananchi wa Kisukuru kuwa tayari walimpa baraka za kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Segerea, akiahidi kuwa amejipanga kwa kiwango cha juu kuhakikisha jimbo hilo linapata maendeleo na usimamizi mzuri wa rasilimali.
6 53 2845
VIDEO:

Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Aida Kenani, amedai kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa ndani na wanachama wa chama hicho na kwamba baadhi yao walikamatwa na kupigwa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV siku ya Jumapili, Kenani amesema mkutano huo wa ndani ulikuwa umepangwa kufanyika katika ukumbi mmoja eneo la Nkasi, lakini akadai kuwa mmiliki wa ukumbi huyo alitishwa na mamlaka na kulazimika kufuta matumizi ya ukumbi huo.

Baada ya hali hiyo, Kenani ameeleza kuwa aliamua kufanya kikao nyumbani kwake na baadhi ya wanachama, lakini akadai kuwa gari za polisi zilifika katika eneo hilo na kuwakamata baadhi ya washiriki, wakati yeye akiwa ametoka eneo hilo. Aidha alidai kuwa baadhi ya waliokamatwa walipigwa.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Shadrack Masija, alipotafutwa na Jambo TV kuhusu madai hayo, alisema yupo mbali na eneo la tukio, lakini atawasiliana na maofisa wa eneo husika ili kupata taarifa kamili juu ya kilichotokea.
229 1373 20162
VIDEO:

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza, amedai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikushinda Jimbo la Segerea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa nguvu yake ya kisiasa, bali kwa sababu ya sintofahamu iliyokuwepo ndani ya vyama vya upinzani vilivyounda umoja wa UKAWA.

Kaiza ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Kisukuru, katika Jimbo la Segerea wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, siku ya Jumapili, katika mkutano wa ndani wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) uliolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenye masuala ya kisiasa.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa tathmini yao, ushindi wa CCM ulikuwa ni matokeo ya upinzani kugawanya kura zake kwa wagombea wawili wa upinzani katika jimbo hilo, siyo kwa sababu wapiga kura walikikataa chama cha upinzani au sera zake.
12 117 6344
VIDEO:

Mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Moza Ally, ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza leo Julai 27, 2025, Moza amesema ana uhakika wa kushinda nafasi hiyo iwapo Chama chake kitampatia ridhaa ya kugombea.

“CHAUMMA kikinipa ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Kinondoni, hakuna mgombea yeyote wa CCM atakayeniweza. Kwa hilo nina uhakika, na ninatuma salamu mapema – wajipange.” amesisitiza Moza
43 227 10757
HABARI PICHA:

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu akipokea nakala tepe ya daftari la kudumu la wapigakura kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Rufani Jacobs Mwambegele kwenye kikao cha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na viongozi wakuu wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mkuu 2025 iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina Dodoma leo tarehe 27 Julai 2025.
19 246
VIDEO:

Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Mhashamu Eusebius Kyando, ametoa wito kwa Watanzania kurejea katika msingi wa kuthamini utu wa binadamu kama nguzo muhimu ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mahafali ya 25 ya Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHET) yaliyofanyika Julai 27, 2025, katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Askofu Kyando amesema kumekuwa na mwelekeo wa kupungua kwa maadili ya utu jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya kijamii.

Mkuu wa Taasisi ya LUHET, Buteye Dotto Buteye, amesema taasisi hiyo inaendelea kuwa chachu ya mafanikio katika sekta ya afya kwa kutoa wahitimu wenye ujuzi, nidhamu na maadili. Ameeleza kuwa serikali imekuwa ikitoa usaidizi mkubwa kwa taasisi hiyo, jambo ambalo limeongeza ubora wa wahitimu wanaoingia kwenye soko la ajira.

Baadhi ya wahitimu akiwemo Roziana Makana pamoja na Willy Mwakajubwa wamesema kutokana mafunzo waliyopata wako tayari kwenda kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya afya na kutii viapo vyao huku pia wakijali utu na haki za wagonjwa.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 320 wametunukiwa vyeti na stashahada mbalimbali katika fani za afya.
21 588 13333
VIDEO:

Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Vernon Fernandes, amesema kuwa serikali imeonesha usikivu na dhamira ya kutatua changamoto zinazolikumba Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, likiwemo suala la kufungwa kwa maeneo ya ibada ya waumini wake.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ibada na waumini wa GCTC Jumapili hii katika Ukumbi wa Kilato Stop Over, Askofu Fernandes amesema kuwa kumekuwa na mazungumzo na serikali juu ya suala hilo, na wamehakikishiwa kuwa hatua za kutatua changamoto hiyo zinaendelea kuchukuliwa.

Askofu huyo ameongeza kuwa japo mchakato wa serikali huchukua muda, tayari wamepata matumaini ya jawabu kwa suala la kufungiwa kwa makanisa hayo, na kwamba wanaamini suluhisho la kudumu litapatikana hivi karibuni.

Baada ya Ukumbi wa Tanzanite kufungwa na mamlaka, waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima siku ya Jumapili wamelazimika kutafuta maeneo mbadala kama Kilato Stop Over ili kuendelea na ibada zao.
53 2749 40405
📍🆕️Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi @ccmtanzania Ndg. Mizengo Pinda, amesema ushirikiano na mshikamano wa vyama sita rafiki vya ukombozi Afrika unapaswa kudumishwa kwa kuzingatia maadili ya ukombozi, misingi ya haki, usawa wa maendeleo jumuishi kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo Ajenda 2063 ya Afrika Tuitakayo.

Pinda aliyasema hayo akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Afrika mjini Gauten, Afrika Kusini. Vyama hivyo sita ni pamoja na ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), ZANU PF (Zimbabwe), FRELIMO (Msumbiji) na Chama Cha Mapinduzi.

Katika mkutano huo ulioanza Julai 25 na unatarajia kumalizika Julai 28, dhima kuu ni kutetea mafanikio ya ukombozi, kusukuma maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi, na kuimarisha mshikamano kwaajili ya Afrika bora. Pinda alisema, mustakabali wa mataifa ya Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Namibia unategemea kwa kiasi kikubwa uhusiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi wake.

Akitoa salamu za CCM kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Pinda alisema vyama rafiki vinawajibika kuhakikisha kuwa vinadumisha mshikamano, maadili ya ukombozi, na misingi ya haki, usawa na maendeleo jumuishi kwa wananchi wote kama ishara ya kutekeleza kwa vitendo Ajenda 2063 ya Afrika tuitakayo, kwa kuwa vimebeba dhima kubwa ya maendeleo.

Alisema umuhimu wa kuwajumuisha vijana katika kila hatua ya harakati za kisiasa na maendeleo ya jamii ni njia muhimu ya kujenga kizazi cha vijana wazalendo, wenye ufahamu wa historia ya vyama hivyo kama ilivyokuwa kwa waasisi wa vyama hivyo ambao walisimama mstari wa mbele katika kujenga vyama hivyo pamoja na kuleta amani kwa mataifa yao.

"Tutakapokuwa na jamii yenye utambuzi wa mchango wa waasisi wa Afrika kama akina Julius Nyerere, Kwame Nkurumah, Nelson Mandela, Sam Nujuma na wengineo kadhalika. Maendeleo ya Afrika yatakuja kwa dhamira ya dhati ya kulinda, kudumisha na kuendeleza misingi ya waasisi wetu ikiwa vijana watakuwa sehemu ya maendeleo hayo." alisema

Alisema mkutano huo ni muhimu katika k
16 131
VIDEO:

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua rasmi wiki tatu za maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), ikiwa ni kuenzi mchango wake katika utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi tangu mwaka 1975.

Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, amesema maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu: “Elimu bila ukomo kwa maendeleo endelevu”, yakilenga kuhamasisha uelewa wa jamii kuhusu nafasi ya elimu ya watu wazima katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Shughuli kuu zitakazotangulia kilele cha maadhimisho ni pamoja na Mafunzo kwa maafisa magereza na wakufunzi wa TEWW, Maonesho ya huduma za elimu ya watu wazima

Kongamano la elimu bila ukomo litakalowakutanisha wadau zaidi ya 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi (Agosti 25–27, Ukumbi wa JNICC).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo, huku Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akitarajiwa kulifunga.

Prof. Mkenda amewahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli hizo ili kupata maarifa na ujuzi unaotolewa kupitia TEWW na wadau mbalimbali, sambamba na kujionea bunifu za vijana na watu wazima wanaopitia mifumo ya elimu isiyo rasmi.
13 75 4281
VIDEO:

Chama cha ACT Wazalendo kimedai kuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeitelekeza sekta ya kilimo na kuwaacha wakulima wakiendelea kuishi katika umasikini na hali ngumu ya maisha licha ya mchango wao mkubwa katika uchumi wa taifa.

Akizungumza siku ya Jumapili Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, ameeleza kuwa hali ya kilimo nchini kwa sasa ni ya kusikitisha na kushangaza, akisisitiza kuwa serikali imekuwa ikiwakumbuka wakulima nyakati za uchaguzi tu kwa ajili ya kuwahadaa na sare za chama, bila kuwa na dhamira ya dhati ya kuboresha maisha yao wala kilimo chao.

Mchinjita ameeleza kuwa kutokana na usimamizi na uwekezaji duni, mauzo ya mazao ya kilimo yameporomoka kwa kiwango cha kutisha. Alichukua mfano wa zao la pamba, ambalo thamani ya mauzo yake imeshuka kutoka dola za Kimarekani milioni 103 mwaka 2023 hadi dola milioni 69 mwaka huu, huku mfumo wa mnunuzi mmoja aliyeidhinishwa na serikali ukishusha bei ya pamba kutoka Shilingi 2,500 hadi 1,200 kwa kilo.

Kwa mujibu wa Mchinjita, hata maeneo yenye mazao yenye soko kubwa kimataifa kama Rungwe na Mbeya, wakulima hawajanufaika ipasavyo. Ameeleza kuwa bei ya chai duniani imepanda, lakini wakulima wa chai wa Tanzania hupata asilimia 10 tu ya bei ya soko la dunia, ukilinganisha na wenzao wa Kenya wanaopata hadi asilimia 60.

Katika kukabiliana na changamoto hizi, ACT Wazalendo imeeleza mkakati wake wa mageuzi ya kilimo iwapo kitapata ridhaa ya kuongoza serikali. Mchinjita amesema chama hicho kitahakikisha sekta ya kilimo inatengewa zaidi ya asilimia 10 ya bajeti ya serikali na kuweka mifumo ya kudhibiti kuporomoka kwa bei za mazao.
25 105 4494